Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, tangu asubuhi ya Ijumaa tarehe 19 Juni 2026, wanamgambo wameimarisha uwepo wao katika maeneo yanayozunguka Msikiti wa Imam Sadiq (as) kwa lengo la kuzuia maandamano ya wananchi yanayofanyika wakati wa maombolezo ya Muharram, vikosi hivyo vilipelekwa katika eneo hilo vikiwa pamoja na magari ya kijeshi na vikosi vyenye silaha.
Licha ya kuwepo kwa mzingiro mkali wa kiusalama, maandamano ya wananchi yalifanyika katika maeneo mbalimbali ya Bahrain. Washiriki wa maandamano hayo walisisitiza msimamo wao wa kupinga kwa nguvu zote udhibiti rasmi wa masuala ya kidini pamoja na vikwazo vinavyoendelea kuwekwa dhidi ya uhuru wa kidini.
Aidha, waandamanaji walilaani hatua za mfumo unaotawala za kuwazuia Mashia kusimamisha Swala ya Ijumaa na pia mashambulizi na ukiukwaji unaoendelea kufanywa dhidi ya shughuli na maadhimisho ya Ashura.
Walitaka kukomeshwa kwa sera za ubaguzi wa kimadhehebu na kuondolewa mzingiro unaowekwa dhidi ya ibada za Mashia.
Vilevile waandamanaji walidai kusitishwa kwa hatua za kuwalenga viongozi wa dini, wanazuoni, taasisi za kidini na misingi ya Madhehebu ya Ja‘fari, pamoja na kuachiwa huru wanazuoni wote wa dini na wafungwa wa kisiasa.
Maoni yako